‘ishu’ ya mashabiki wa Simba na Yanga kushangilia wapinzani wa nje pindi timu hizo zinapokuwa zinacheza mechi za kimataifa kumbe ni kero pia kwa Katibu Mkuu wa Yanga Charles Boniface Mkwasa.
Mkwasa amesema jambo hilo ni miongoni mwa vitu vinavyomkera kuhusu timu za Simba na Yanga.
“Kitu ambacho huwa kinanikosesha raha kuhusu hizi timu mbili za Simba na Yanga ni kwamba, vita vyetu sisi ilitakiwa vibaki humu ndani lakini inapokuja suala la uwakilishi nadhani tungekuwa nguvu moja kitu ambacho wenzetu wanafanya.”
“Wanatucheka sana wenzetu wanaokuja hapa halafu wanapata mashabiki hapa, duniani kote hakuna ni Tanzania tu halafu tunataka kuendelea, tutaendeleaje namna hii?
“Nafikiria kwamba ushabiki wetu ubaki palepale lakini ikifika kwenye suala hili kama wewe hutaki bora ukae nyumbani, sio unakwenda uwanjani kusapoti timu ngeni.”
“Mfano imetokea vita kati ya DR Congo na Tanzania wanakuja maadui wa Congo kutaka kuuwa wanajeshi wa Tanzania wewe unashirikiana na wale badala ya kusaidia nchi, sasa sijui hiyo vita itakuwaje.”
Afisa habari wa Simba Haji Manara amewahi kuzungumzia jambo hilo kabla ya kuanza kwa mechi za kimataifa msimu huu. Manara aliwaambia mashabiki wa Simba wasizomee wala kushangilia wapinzani Yanga itakapokuwa ikicheza mechi yao ya kimataifa.
No comments:
Post a Comment